The House of Favourite Newspapers

Watanzania 13 Wafariki kwa Ajali Uganda

0
Ajali ilivyotokea.
WATANZANIA 13 wamefariki na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika eneo la biashara Lubanda takribani kilomita 80 kufika Kituo cha Polisi cha Fika Salama karibu na Mto Katonga Wilaya ya Mpigi, Kampala, Uganda.
Ajali hiyo imehusisha  gari aina ya fuso yenye namba za usajili UAH 970P na coaster yenye namba T540 DLC waliokuwa wakitumia Watanzania hao wakiwemo ambao inasemekana walikuwa wakitoka kwenye  harusi ya binti wa Dkt. Annette Ibingira ambaye ni mke wa mhazini wa shule ya Wazazi ya Kampala nchini Uganda Dkt. Ibingira.
Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Nkozi na Double Cure Clinic zilizopo nchini Uganda huku miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo imepelekwa katika Hospitali ya Gombe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera, Augustine Ollomi amethibitisha kupokea taarifa za ajali hiyi na kusema Watanzania hao walikwenda Uganda kwa ajili ya shughuli ya harusi lakini hana taarifa walikwenda sehemu gani nchini humo. Amesema wanaendelea kufanya mawasiliano na mamlaka za Uganda kujua undani wa ajali hiyo.

“Ni kweli tumefuatilia basi hilo na kubaini kwamba liliondoka hapa nchini Septemba 15 kwenda Uganda kwenye shughuli ya harusi. Mengine siwezi kusema zaidi mpaka tutakapofanya mawasiliano na mamlaka za Uganda,” amesema Ollomi.

INAUMA SANA! Mama Asimulia Saa za Mwisho za Mwanaye kabla Hajatekwa na Kuuawa

Leave A Reply