The House of Favourite Newspapers

Miili ya Watoto 3 Waliolipukiwa na Bomu Yaagwa

0
Majeneza yenye miili ya marehemu yakiingizwa kwenye gai kupelekwa kijijini kwa mazishi.

MIILI ya watoto watatu waliofariki dunia kwa mlipuko wa bomu kwenye eneo la mazoezi ya kijeshi wilayani Monduli, mkoani Arusha imeagwa leo kusafirishwa kwa maziko katika Kijiji cha Nafco.

 

Majeneza yenye miili ya marehemu.

Shughuli ya kuaga miili hiyo imefanyika leo Jumatatu katika Hospitali ya Wilaya ya Monduli.

 

Majeneza yenye miili ya marehemu yakiingizwa kwenye gai kupelekwa kijijini kwa mazishi.

Watoto hao walifariki dunia Ijumaa jioni katika Kijiji cha Nafco kilichopo Kata ya Loksale walipokuwa wakichunga ng’ombe.

 

Majeneza yenye miili ya marehemu.

Ilielezwa watoto hao walilipukiwa na bomu walipokuwa wakilichezea wakidhani ni mpira.

 

Majeneza yenye miili ya marehemu.

Watoto hao wametajwa kuwa ni Johnson Daniel, Lendisi Saitabau na Samweli Nyangusi.

Nguo za watoto hao.

Mkuu wa Wilaya ya Monduli, Idd Kimanta ameongoza kamati ya ulinzi na usalama kuaga miili ya watoto hao.

Majeneza yenye miili ya marehemu yakiingizwa kwenye gai kupelekwa kijijini kwa mazishi.

 

NA HILALY DAUDI | GPL

Leave A Reply