The House of Favourite Newspapers

Watanzania 725 Wafariki kwa Corona – Video

0

WATANZANIA 725 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa Uviko-19 tangu ulipoingia nchini mapema mwaka jana. Idadi hiyo ni kati ya watu 26,164 waliothibitika kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo kati ya hao 25, 330 walipona.

 

Takwimu hizo zimetolewa leo Jumatano Novemba 10, 2021 bungeni na Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel wakati anajibu swali la mbunge wa viti Maalum Halima Mdee.

 

Katika swali la msingi Mdee ameuliza ni Watanzania wangapi wameugua Uviko-19 tangu ulipoingia nchini na akahoji Fedha kiasi gani zimetumika.

 

“Sh158 bilioni zimetumika kununua vifaa mbalimbali ikiwepo mitambo 19 ya kuzalisha hewa ya oksijeni yenye uwezo wa kuzalisha mitungi 20 hadi 300 ambapo mitambo saba ishasimikwa na mitambo 12 ipo katika hatua ya usimikaji,” amesema Naibu Waziri Mollel.

 

Akizungumzia gharama za upimaji amesema kipimo kwa mtu mmoja ni dola 135 ambapo Serikali inatoza dola 50 huku ikichangia dola 85 kwa kila anayepima.

 

Leave A Reply