Watu 73 Washikiliwa Na Polisi Kesi Ya Mauaji, Madawa Ya Kulevya – Video
Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu, kupitia Opereisheni iliyoanza Mei, 01, 2023 hadi Mei 24, 2023 imefanikiwa kuwadaka watu 73 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya mauji, wizi wa mifugo, uvunjaji, pamoja na madawa ya kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe akizungumza na waandishi wa Habari leo Ofisi kwake, amasema kuwa baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa wamefikishwa mahakani huku wengine upelelezi dhidi ya makosa yao ukiendelea.