The House of Favourite Newspapers

Dozi Bil. 1 za Covid- 19 Zatolewa China

0

CHINA imetangaza  kwamba imefikisha jumla ya Dozi bilioni moja za   chanjo dhidi ya COVID-19 kufuatia kampeni yake kubwa kabisa ulimwenguni ya utoaji chanjo.

 

Maafisa wa afya nchini humo wanapanga kuchanja asilimia 40 ya Wachina ifikapo mwisho wa mwezi huu, baadhi ya mikoa inatoa chanjo bila malipo kama njia ya kuwahimiza watu kujitokeza kuchanjwa.

 

Katika mikoa mingine kama Anhui ya kati watu vyakula bila malipo na katika maeneo mengine ya mji wa Beijing watu wanapewa vocha za kununua bidhaa ikiwa n sehemu ya kuwashawishi watu kupata chanjo hiyo.

 

Hayo yanajiri mnamo wakati nchini Brazil, idadi ya vifo kufuatia janga hilo imepita watu nusu milioni,Ulimwenguni kote, idadi ya vifo kutokana na janga la COVID-19 imepita milioni 3.8.

 

Leave A Reply