The House of Favourite Newspapers

Watu Wazidi Kumchangia Jini Kabula

1
Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’.

MUDA mfupi baada televisheni ya mtandaoni inayoongoza kwa kutazamwa na wat wengi zaidi ya Global TV Online kujitokeza kuendesha kampeni maalum ya kumchangia fedha za kusaidia matibabu na huduma kwa mwigizaji Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ ijulikanayo kwa Jina la Support Jini Kabula For Treatment, watu wengi wameendelea kuguswa na suala hilo hivyo kuanza kujitolea kwa moyo kwa kadiri walivyojaliwa.

 


Kwa nyakati tofauti, baadhi ya watu hao walizungumza na mwandishi wetu kupitia simu ya mkononi ambapo walieleza hisia zao namna ambavyo wameguswa na tatizo la Kabula baada ya kutazama mahojiano yake kupitia Global TV Online.

 

“Binafsi nimeguswa sana na tatizo la Kabula hivyo kwa chochote nitakachojaliwa nitajitolea kwa ajili ya kusaidia, naamini na wengine wataguswa kama mimi, maana najua Watanzania tuna moyo wa upendo na mshikamano kwenye matatizo,” alisema mmoja wa wadau waliozungumza na mwandishi wetu.

Kwa mujibu wa ndugu wa Kabula, kwa mtu yeyote anayeguswa na tatizo la ndugu yao na yupo tayari kujitolea kumsaidia kwa chochote, basi atume mchango wake kupitia simu ya mkononi kwa namba: 0712 56 53 69 ambapo jina litasomeka Daynes Jolwa ambaye ni dada wa damu wa Jini Kabula.

 

Kutoa ni moyo si utajiri. Kwa chochote kidogo, tujitoleeni kumsaidia msanii huyu kwani matatizo huzunguka, leo kwake, kesho unaweza kuwa wewe au ndugu yako. Asanteni na Mungu awabariki sana-Global TV Online.

 

STORI: BRIGHTON MASALU, DAR

1 Comment
  1. […] MWANADAMU hakipendi kifo. Katika kuhakikisha anaendelea kuishi, hupambana kwa kila hali ili aendelee kubaki salama. Miongoni mwa njia zinazotumiwa kujihakikishia miaka mingi ya kuishi, ni kufanya mazoezi na kula vizuri. Hayo ndiyo yafanywayo na watu duniani kote. Pamoja na harakati zote hizo, yapo mataifa ambayo kwa wastani watu wake huishi miaka mingi zaidi ukilinganisha na mataifa mengine. Katika orodha hii, uta-zifahamu  nchi nne ambazo watu wake huishi miaka mingi, zipo siri zinazofanya waweze kudumu kwa muda mrefu: […]

Leave A Reply