The House of Favourite Newspapers

Wazungu Wawawekea Mamilioni Mastaa Bongo

0

HII inaweza kuwa good news kwa mastaa Bongo! Wazungu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wamewatengea mamilioni ya shilingi, mastaa wanaozalisha kazi mbalimbali za sanaa Bongo, IJUMAA WIKIENDA linakupa mchongo kamili.

 

WENGI HAWAJUI…

Habari iwafi kie, moja kati ya vitu ambavyo kumbe wasanii wengi hawavijui ni kwamba, wamewekewa mamilioni hayo ambayo wanayapoteza kwa kutokujua jinsi gani wanaweza kuyapata.

 

UCHUNGUZI UMEFANYIKA

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limefanya uchunguzi na kubaini kwamba, kuna platforms (mitandao ya kuuza, kupakua, kusikiliza na kutazama muziki) zilizoanzishwa na Wazungu mbalimbali, ambazo zina uwezo wa kuwaingizia mastaa pesa kwenye akaunti zao kila mwezi, endapo wakizijua na kufuata taratibu zote za kujiunga.

 

Uchunguzi umebaini, mastaa wanaofanya vizuri kwa upande wa Bongo Fleva na Bongo Movies kama Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Rajabu Abdul ‘Harmonize’, Zuhura Othman ‘Zuchu’ na Faustina Charles ‘Nandy’ wanaoweza kujiingizia mamilioni hayo, kama watashtuka.

 

Wengine ambao pia wanaweza kuitumia fursa hiyo, ni pamoja na Maua Sama, Hamisa Mobeto, Wema Sepetu, Irene Uwoya, Vincent Kigosi ‘Ray’, Jacob Steven ‘JB’ na wengineo.

 

TUMSIKILIZE MTAALAM

Akizungumza na IJUMAA WIKIENDA, mtaalam wa mambo ya IT (Information Technology), Edwin Lindege, alisema kuwa wasanii wengi wanakufa masikini kwa kutokujua kama wana uwezo wa kuingiza pesa kila mwezi hata kama ikitokea hajafanya shoo kwa miezi kadhaa.

 

“Platforms ambazo zinawaingizia pesa wasanii wa muziki nchini, zipo nyingi sana, zinaweza kufi ka hata 200, lakini kwa ufupi tu, nitazitaja zile ambazo ni common (zilizozoeleka) mfano kuna Mtandao wa YouTube (mmoja wa waanzilishi wake ni Jawed Karim) Itunes, Deezer, Audiomack, Boomplay, Spotify, Google Play Music, Apple Music, TargetMusic, Vevo, Amazon (imeanzishwa na tajiri namba moja duniani, Jeff Bezos) na nyinginezo.

 

“Lakini pia wasanii wanatakiwa kufahamu kwamba, kujiunga katika platform zote hizi ni bure, ila inategemea mhusika anajiunga kupitia wapi. Kama haelewi, basi anaweza akapigwa pesa hata milioni tano mpaka kumi hivi.

 

“Jambo lingine ni kwamba, ili uweze kupata hizo pesa, basi unatakiwa uwe na fun-base ya mashabiki wa kutosha na siyo viewers (watazamaji), kwa sababu wao wanachoangalia ni ubora na uzuri wa wimbo wako, streaming au watch time kwa YouTube (muda wa kutazamwa au kusikilizwa) lakini pia na namna ilivyo-trend (kubalika).

 

“Pia hizo platforms, huwa unatakiwa uwe na viewers kadhaa, ili waanze kukuingizia pesa, mfano kama YouTube unatakiwa uwe na kuanzia subscribers 1,000, muda wa kutazamwa (watch time) saa 4,000 ndani ya miezi 12, ndiyo wataanza kukuingizia pesa na kuhusu wao kujua una viewers wangapi ili waanze kukulipa, ni suala jepesi kwao, kwa sababu ukishajiunga, moja kwa moja watatambua una viewers wangapi kwenye akaunti yako,” alisema mtaalam huyo.

 

NINI KIFANYIKE?

Mtaalam huyo anaendelea kueleza kwamba, asilimia kubwa ya mastaa tulionao Bongo, wachache ndiyo wanajua jinsi ya kutumia hizo platforms na wengi wao hawajui, akimtolea mfano Diamond, kuwa ni msanii ambaye anaweza asifanye shoo hata miezi miwili, lakini kipindi chote hicho, pesa zikawa zinaingia kwenye akaunti yake.

 

Hivyo na kwa wasanii wengine, wanatakiwa waamke na kujua jinsi ya kuitumia hii mitandao ili waepukane na umasikini kwa kutafuta watu professional (wataalam) wa hayo mambo, wawaeleweshe ili iwe rahisi kwao kunufaika badala ya ‘kupigwa’.

 

“Wanachotakiwa kufanya wasanii ili wawe wanaingiza pesa kupitia hii mitandao, ni kutafuta wataalam ambao wana uelewa wa hizi platforms ili waweze kupiga pesa.

 

“Lakini kama ikitokea wameshindwa kuwapata hao wataalam, basi ni vyema pia wakakutana na wasanii wenzao ambao tayari wanatumia hii mitandao, wawaulize jinsi wao wanavyoitumia ili na wao waweze kunufaika nayo,” alisema.

 

Mathalan, kwa mtandao wa YouTube peke yake, Mondi anaingiza si chini ya Dola 7,600 (Sh.17, 634, 006) mpaka 12,300 (Sh. 28,539,247) kwa mwezi, sawa na Dola 91,000 (Sh. 211,144,024) hadi 1,500,000 (Sh. 3,480,396,000) kwa mwaka.

STORI: MEMORISE RICHARD, DAR

Leave A Reply