The House of Favourite Newspapers

Wawili Wafariki Katika Maandamano ya Uchaguzi Kenya

0
Mawe yakiwa yamepangwa barabarani wakati polisi wakiimarisha usalama.

 Watu wawili wameuawa wakati wa vurugu wakikabiliana na maofisa wa polisi katika ngome ya upinzani ya Mathare, Mji Mkuu wa Nairobi nchini Kenya.

Risasi zikilindima.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa walisikia milindimo ya risasi zikifyatuliwa wakati wa makabiliano hayo ambayo yalisababisha vifo hivyo.

 

Polisi wakituliza ghasia.

 Afisa Habari wa Shirika la Habari la Ufaransa, Agence France-Presse (AFP), limeeleza kuwa, waliouawa walikuwa miongoni mwa kundi la waandamanaji katika eneo hilo ambao walikuwa wakipambana na kikosi maalum cha kuzuia ghasia hizo.

 

Hali ilivyokuwa.

”Tumeambiwa kwamba wengi wao walikuwa wezi ambao walitumia fursa hiyo na hawakuweza hata kuwaheshimu polisi”, alisema ofisa huyo.

Askari wakituliza ghasia.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga amesema kuwa uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu ili kumpokonya ushindi.

Mataili yakichomwa barabarani.

, Saa Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais kufikia sasa

Katika matokeo ya awali ya vituo 39091 kati ya 40883 yaliyopakiwa na IEBC mtandaoni:

  • Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,977,905 (54.32%)
  • Raila Odinga wa ODM ana kura 6,578,586 (44.79%)

Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 387,959.

 HABARI TBC 1: Matukio Yote ya Siku (Agosti 9) 

Leave A Reply