The House of Favourite Newspapers

Waziri Gwajima: Watoto Hawaruhusiwi Kucheza ‘Show’ Kwenye Sherehe Usiku

0
Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

Kufuatia kusambaa kwa Video iliyowaonesha Watoto wakitoa Burudani kwenye Sherehe wakati wa Usiku na katika Miondoko isiyofaa kwa Umri wao, Waziri Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewatafuta Wazazi wa Watoto hao na kukemea kitendo hicho huku akiwataka Washereheshaji na Jamii kuzingatia Sheria inayokemea Udhalilishaji wa Watoto

Sheria ya Mtoto Namba 21 ya Mwaka 2009 (iliyorekebishwa Mwaka 2019), kifungu cha 158 (1) (c) inazuia kumtumia Mtoto kwenye Maonesho ya Harusi, Maonesho ya Mitindo ya Nguo au Maonesho mengine kama hayo wakati wa Usiku. Adhabu yake ni faini ya Tsh. Laki 5 au kifungo cha Miezi 6 jela au vyote kwa pamoja.

BABA MZAZI wa WARDA (15) ALIYEPOTEA AKIWA KWA MKUU wa SHULE AANGUA KILIO STUDIO | MAPITO

Leave A Reply