The House of Favourite Newspapers

Waziri Mkuu Agusa Makubwa Ya Rais Dkt. Samia Katika Kipindi Cha Miaka Mitatu

0

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania imeshuhudia magaeuzi na maboresho makubwa ya kiuchumi, kijamii na kisiasa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Sukuhu Hassan.

Amesema kuwa matokeo ya jitihada hizo ambayo kwa kiasi kikubwa yameimarisha ustawi wa Watanzania yanapaswa kuungwa mkono na kila mtanzania bila kujali itikadi ya vyama vyetu. “Kazi yake kubwa tumeiona, matunda ya kazi yake yamekuwa na manufaa kwetu sote”

Amesema hayo Jumatano, Machi 27,2024 wakati wa Kongamano la Kurasa 365 za Samia lililoratibiwa na Kampuni ya Clouds Media kwenye ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo lililenga kuonesha mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Madarakani.

Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia katika kipindi cha miaka mitatu ameendeleza miradi yote ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), ujenzi wa Bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere ambalo limeanza kuzalisha umeme na kuingiza katika gridi ya Taifa, uendelezaji wa mji wa Serikali

Miradi Mingine ni Ujenzi wa Madaraja Makubwa ya Mfano ikiwemo Kigongo-Busisi ambao ujenzi wake umefikia asilimia 85 na Ujenzi wa Meli ya MV. Mwanza “Hapa Kazi Tu” ambayo ujenzi wake umefikia asilimia 93 na imeshaanza majaribio.

Amesema kuwa Rais Dkt. Samia ameendelea kuwa kinara katika kuendeleza diplomasia ya uchumi ambayo kwa yameiwezesha Tanzania kupanua wigo wa uwekezaji “Kitendo hiki cha Rais Dkt. Samia kuhamasisha mataifa ya nje kujenga urafiki wa karibu na Tanzania yametuwezesha kufanikiwa kwenye maeneo ya utalii uwekezaji, mitaji, masoko ya bidhaa, ongezeko la watalii, na utatuzi wa changamoto za kibiashara na nchi jirani”

Akizungumzia Sekta ya Elimu Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa kwa sasa Serikali inakamilisha ujenzi wa shule za msingi katika kila kijiji kwa lengo la kumuwezesha mtoto wa Kitanzania atembee umbali mfupi kufuata shule “Sekondari tulianza na mpango wa kata na tunaendelea kuongeza shule”

#EXCLUSIVE: WEMA SEPETU -”SIPENDI MISIBA WALA BABY SHOWER – NAJISIKIA VIBAYA – MOYO WANGU MWEPESI”strong>

Leave A Reply