The House of Favourite Newspapers

Mpango Amwaga Chozi Akitoka Hospitali -Video

0

WAZIRI  wa Fedha na Mipango, Dk. Phillip Mpango, leo Februari 23, 2021, ameruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma, ikiwa ni siku chache baada ya kuzushwa kwamba amefariki dunia.

 

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo muda mfupi baada ya kuruhusiwa, Dk. Mpango amesema afya yake kwa sasa ni imara, tofauti na siku chache zilizopita ambapo alifikishwa hospitalini hapo akiwa na mitungi ya hewa ya Oksijeni.

 

Dk. Mpango amesema anamshukuru Mungu kwa miujiza aliyomtendea kwa siku 14 alizokuwa anapigania uhai wake, lakini pia ameeleza kuwa anamshukuru sana Rais Dk. John Magufuli ambaye alikuwa akimjulia hali kila siku, viongozi wa kiserikali pamoja na viongozi wa kidini pamoja na watu wengine wote waliokuwa wakimuombea katika kipindi kigumu alichokuwa anapitia.

 

“Leo ni siku ya 14 tangu nije hapa Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma, nilikuja na mtungi kabisa wa kupumulia. Leo ni siku ya 3 situmii mtungi namshukuru Mungu amenitendea makubwa kutoka nilikokuwa madaktari wakinihudumia nyumbani mpaka hapa, acheni Mungu aitwe Mungu.

 

 

“Namshukuru Rais Magufuli kwa upendo wake, hakuna siku ambayo hakunipigia simu kunijulia hali. Viongozi wa Hospitali hii ya Mkapa wamekuwa wakifuatilia hali yangu kila siku, Makamu wa Rais, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu, Spika na wananchi wote kwa kuniombea.

 

“Natoa pole kwa waliopoteza wapendwa wao katika wiki hizi mbili, ningefurahi kushiriki lakini sikuweza, Mhe. Maalim Seif, Balozi Eng. Kijazi, nimempoteza mwalimu wangu wa pekee, Prof. Benno Ndulu, mdogo Mhe. Nditiye, namuomba Mungu awape pumziko la milele.

 

 

“Ninarudi kazini, kazi ndogondogo nimeshaanza kufanya, nawasihi tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu, atatuvuisha, amenivusha mimi na ninaamini wagonjwa wenzangu niliowaacha hapa watatembea kwa afya kama mimi.

 

 

“Magonjwa yapo mengi, sio mara ya kwanza ninabanwa na kifua, mdogo wangu Nditiye amekufa kwa ajali, vifo vipo vingi, tuondokane na hofu iliyotanda, Mungu yuko pamoja nasi,” amesema Dkt. Mpango.

 

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8

⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

 

 

Leave A Reply