The House of Favourite Newspapers

Spoti Xtra Lamwaga Tiketi za Simba vs Al Ahly

0

TIMU ya Masoko kutoka Kampuni ya Global Group ambao ni wachapishaji wa magazeti namba moja kwa habari za michezo kupitia gazeti la Spoti Xtra imeingia mtaani leo Februari 23 kutoa zawadi kwa wateja wake.

 

 

 

Ziara ya leo ilikuwa ni maeneo ya, Buguruni, Tandika na maeneo ya Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ambapo kuna tukio la mchezo wa kukata na shoka timu ya Simba inayocheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika watakapocheza dhidi ya Al Ahly ya Misri.

 

 

 

Mchezo huo wa Kundi A, unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.

 

 

 

Anthony Adam, Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji kutoka Global Publishers amesema kuwa ni kawaida ya kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wasomaji wake ikiwa ni pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali.

 

 

 

“Hii imekuwa desturi yetu kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu kwani wamekuwa wakituunga mkono, hivyo ni jambo jema kuwarudishia kile tunachokipata kutoka kwao, kwa kuwa sote ni familia ya Spoti Xtra.

 

 

 

“Wasomaji wetu tuliowakuta wakiwa na nakala ya gazeti la Spoti Xtra tumewapa tiketi ya kuingilia kwenye mechi hiyo, hii imekuwa ni kawaida yetu kuwapa tiketi wasomaji wetu wanaokutwa wakiwa na nakala ya gazeti,” amesema.

 

 

 

Leave A Reply