The House of Favourite Newspapers

LIVE: Waziri Ummy Azindua Ujenzi wa Kiwanda cha Dawa za Binadamu Bagamoyo

TAZAMA TUKIO ZIMA LIVE HAPA


Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Pwani, Happines Seneda akifungua hafla hiyo ndani ya Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo kwenye Hoteli ya Oceanic, Bagamoyo.

Watanzania Wazalendo wameamua kutatua changamoto ya mueda mrefu ya upatikanaji wa dawa hapa nchini baada ya kuamua kujenga Kiwanda kikubwa cha kutengeneza dawa za binadamu ambacho mitambo yake itasimikwa eneo la Zinga wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.

Eng.  Holger Link kutoka Ujerumani ambaye ni mshauri mkuu  wa Zinga  Pharma Ceuticals.

   

Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza kabla ya kuanza hafla hiyo.

Kiwanda cha Zinga Pharmaceuticals LTD ambacho uzinduzi wa ujenzi huo unatarajiwa kufanywa leo Machi 30, 2017 na Mgeni Rasmi ambaye ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Watoto Jinsia na Wazee, Mhe. Dkt. Ummy Mwalimu, kitatengeneza dawa zenye standard ya Europe na kitakuwa na uwezo wa kusambaza dawa hizo Afrika Mashariki na Kati.

Mbunge wa Bagamoyo, Shukuru  Kawambwa akiwakaribisha wageni kwenye hafla ya uzinduzi huo.

Mitambo itakayozalisha dawa hizo itatoka Ujerumani na tayari wataalam wake wameshaingia nchini kwa ajili ya kuanza kufanya kazi hiyo muhimu.

Dkt. Marry Mayige akielezea kwa wageni mipangilio ya Zinga Pharma Ceuticals watakavyotumia utalam wao kuzalisha dawa nyingi za Kitanzania zenue viwango vya kimataifa.

Wadau wa mradi huo katika picha ya pamoja.

Mitambo hiyo itagharimu pesa za Kitanzania Shilingi bilioni 70 kwa ajili ya kutengeneza dawa za binadamu.

Imeandikwa na Edwin Lindege

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaa, muziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.