The House of Favourite Newspapers

Waziri wa Nishati Prof. Muhongo Asimamisha Bei Mpya za Umeme

WAZIRI mwenye dhamana ya kusimamia Nishati na Madini hapa nchini, Prof. Sospeter Muhongo, leo Desemba 31, 2016 amesimamisha mara bei mpya za manunuzi ya umeme zilizopitishwa na kutangazwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), kuwa bei ya umeme itapanda kwa asilimia 8.5% ifikapo Januari 2017.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi jana, ongezeko hilo la bei ni kufuatia maombi ya Shirika la Umeme nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19.

Ewura Kupandisha Bei ya Umeme 8.5% Kuanzia Januari

Taarifa iliyotolewa leo na Waziri Prof. Muhongo imeitaka EWURA kusitisha mara moja utekelezwaji wa mpango huo wa kuongeza asilimia 8.5% ya bei ya umeme, na badala yake isubili maamuzi mengine ya serikali itakapojiridhisha baada ya kupitia ripoti rasmi zote zitakazowasilishwa na EWURA, ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wadau wote wa masuala ya nishati.

bei-ya-umeme-tanesco

Comments are closed.