The House of Favourite Newspapers

Wema Akwaa Kesi Nzito ya Kudaiwa

0

STAA mkubwa wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu anadaiwa kukwaa na kesi nzito ya kudaiwa deni kubwa na Wakenya, lakini yeye mwenyewe ameliambia Gazeti la IJUMAA; “Nimechoka kusakamwa!”Kwa mujibu wa walalamikaji ambao ni madakatri alioingia nao kwenye mkataba wa kimatibabu wakihusika na kumfanyia upasuaji, walikubaliana na kuingia mkataba kwamba, kama jambo lake litafanikiwa la kupungua kilo alizohitaji, basi awe balozi wao.

 

Lakini inadaiwa kwamba, baada ya jambo lake kutimia, Wema ambaye ana wafuasi mamilioni kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, aliingia mitini na siku zikazidi kuyoyoma.Hata hivyo, inasemekana kilichowaibua madaktari hao ni baada ya Wema kuendelea kukanusha kwamba hakufanyiwa upasuaji wala kutumia dozi yoyote, bali alifuata utaratibu wa dayati na mazoezi ya kujipunguza mwili.

 

Pia Wema ameendelea kusisitiza kuwa, safari yake ya India ilikuwa ni kwa ajili ya matatizo yake mengine ya tumbo.Lakini wenyewe madaktari hao wanashikilia msimamo wao kwamba, wao ndiyo waliomsafirisha Wema kwenda nchini India kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa kupunguza unene unaoitwa ‘biometric’.

 

Madaktari hao wanadai kuwa, chini ya mkataba wao na Wema, waligharamikia upasuaji wa kumsaidia kupunguza uzani wa mwili naye awafanyie matangazo ya kibiashara kama balozi wake.

Madaktari hao walitimiza jukumu lao, ghafla Wema alionekana amepungua mwili, lakini hakusema ukweli kuhusu namna aliyotumia kufikia mwili wake mdogo.Sasa kampuni hiyo ya madaktari ya Kenya inadai ‘kufaili’ kesi hiyo wakidai Wema awalipe gharama zao.

 

Hata hivyo, katika mahojiano na Gazeti la IJUMAA, Wema anasema kuwa, watu wamuache kidogo kwani amechoka kusakamwa.“Hebu kwanza watu waniache kidogo jamani kwa sababu kila mara nazungumziwa mimi tu? Mimi mwenyewe nitaweka wazi kila kitu wala watu wasiongee tu,” anasema Wema.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

PAULA AKIRI Mbele ya MAMA YAKE – “MARAFIKI WAMENIKIMBIA, NATAMANI NISINGEKUWA PAULA”

Leave A Reply