The House of Favourite Newspapers

Wema Amrudia Mungu

0

 

STAA mwenye nyota zake Bongo, Wema Sepetu amesema baada ya mapito ya muda mrefu amebadili mfumo wake wa maisha na kwamba anafanya dua na kumtegemea Mungu katika mambo yote.

 

Wema anasema pamoja na kubadili mfumo wa maisha yake, bado ni yuleyule, hajawahi kubadilika na anaamini katika kupata kwa wakati sahihi wa Mungu na sasa anaona huo wakati wake umefika.

 

“Mimi ni binti wa Kiislam nafanya sana dua. Watu wanamuona Wema wa mtandaoni, lakini binadamu tunakuwa na tunajifunza, tunaoamini katika Mungu, Mungu hukupa kwa wakati wake na wakati ambapo hakunipa aliwapa wengine, riziki inaenda kwa mzunguko,” anasema Wema.

CC; @sifaelpaul

Leave A Reply