Wema amtusi Diamond

WEMA40.JPGWema Sepetu akiwa ndani ya gari lake jipya.

STORI: MUSA MATEJA NA IMELDA MTEMA

WEMA Isaac Sepetu ‘Madam’ ameangusha bethidei baab’kubwa ambayo imesheheni kufuru ya aina yake na ‘kumtusi’ hadharani mpenzi wake wa zamani, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kumsema kuwa ni mtu wa kununua magari ya bei rahisi hivyo hawezi kuifikia hadhi yake, Risasi Mchanganyiko lina mchapo kamili.

Diamondss-2.jpgStaa wa Bongo Fleva Nasibu Abdul ‘Diamond’.

ILISOGEZWA MBELE MAKUSUDI

Sherehe hiyo ambayo ilikuwa ifanyike Septemba 28, mwaka huu ambayo ndiyo siku ya kuzaliwa Madam, ilisogezwa mbele makusudi kutokana na ubize aliokuwa nao wa kukifanyia kampeni Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuamua kuifanya Jumapili iliyopita (Novemba 1) baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo iliyoisha kwa ushindi wa mgombea urais wa CCM Dk John Magufuli.

WEMA23.JPGENEO LA TUKIO

Sherehe hiyo iliyosheheni mastaa kibao Bongo, ilifanyika katika ukumbi wa Wema Sepetu uliopo ndani ya jengo la Millenium Towers, Kijitonyama jijini Dar ambapo mwanadada

huyo alizua gumzo la aina yake baada ya kujizawadia gari aina ya Range Rover lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200.

WEMA27.JPG
Staa wa Bongo Fleva, Ali Kiba.

MASTAA WAANGUSHA BURUDANI

Mbali na kusheheni vyakula vyenye hadhi ya juu, kwenye sherehe hiyo walikuwapo mastaa mbalimbali wa Bongo Fleva kama Barnaba Elias, Ali Kiba, Vanessa Mdee na Sam Machozi ambao walitumbuiza nyimbo mbalimbali kusherehesha pati hiyo.

WEMA5.JPGWema Sepetu.

KEKI ZA KUMWAGA

Kuonesha kwamba amedhamiria kuwakomesha, keki kubwa kwenye sherehe hiyo zilikuwa tano sambamba na ndogondogo zaidi ya 20 ambazo zilipambwa katika meza aliyokaa Wema na kuvutia.

MAVAZI MEUPE YATAWALA

Waalikwa kwenye sherehe hiyo walionekana kufunikana kwa kuvaa mavazi meupe yenye mvuto wa tofauti hivyo kuufanya ukumbi mzima kuonekana mweupe.

WEMA35.JPGMartin Kadinda ambaye ni Meneja wa Wema Sepetu, akimwonesha ramani ya nyumba.

ZAWADI SASA

Ulipofika wakati wa zawadi, mastaa na waalikwa mbalimbali walishindana kumtunza mrembo huyo asiyechuja Bongo, vitu mbaimbali vya thamani, zikiwemo fedha taslimu ambapo ‘wekundu wa Msimbazi’ walionekana kutapakaa katika eneo maalum la kupokelea zawadi alilokaa Madam.

AMTUSI DIAMOND

Mara baada ya kukamilika kwa zoezi la zawadi ndani ya ukumbi, ndipo Wema alipowatoa nje waalikwa na kuwaonyesha gari lake jipya aina ya Range Rover ambalo linasadikika kuwa litakuwa la kwanza kumilikiwa na msanii wa kitanzania kutokana na thamani yake.

“This is my new brand car, yaani ni mpya ya mwaka 2015, hakuna kenge yeyote anayeweza kufuata nyendo zangu na yule ambaye alikuwa akijigamba eti alinipa zawadi ya gari la elfu 30, nini na nini na hili aseme sasa maana mimi si wa kuhongwa kila kitu,” alisema mrembo huyo, kauli iliyoonyesha wazi kumlenga Diamond, ambaye aliwahi kumzawadia Wema gari lenye thamani ya shilingi milioni 30 miaka michache iliyopita.

WEMA37.JPGGari aina ya Range Rover alilonunua Wema.

AANIKA GHARAMA ZA GARI

“Naomba niwaambie kuwa hadi naifikisha hapa, hii gari nimetumia zaidi ya dola elfu 90 za Kimarekani, sijahongwa na mtu, ni pesa yangu kwa nguvu zangu mwenyewe, nawaomba mpande ndani mshuhudie ziro kilometa (halijatumika).

NI GARI LA NDOTO ZAKE

kwa hatua hii maana ilikuwa ni gari ya ndoto zangu, na leo namshukuru Mungu yangu mwenyewe, hakuna anayeweza kugusa hapa inaitwa piga kimya, ni mpya ambayo natarajia kuanza kuchana karatasi zake kuanzia kesho,” alisema Madam.

WEMA17.JPGWATU WAMPIGIA SALUTI

Baadhi ya waalikwa ambao walishuhudia shughuli hiyo na mama mzazi wa mrembo huyo Miriam Sepetu, kusema ameandaa hafla ya kistaa, ambayo inaendana na hadhi yake.

“Daah kuanzia ukumbi ulivyopambwa, gari alilojinunulia, vyakula na vinywaji ni balaa. Hakuna mfano sijaona pati ambayo wahudhuriaji.

WALIOHUDHURIA

Sherehe hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wa burudani, ilipambwa na mastaa wengi akiwemo mtangazaji Hamis Mandi ‘B 12’, Idriss Sultan, Martin Kadinda, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Halima Yahya ‘Davina’ na Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.


Loading...

Toa comment