The House of Favourite Newspapers

Wema Sepetu Kortini Tena Kesi ya Kusambaza Picha za Ngono – Video

Msanii wa filamu za Bongo Movies, Wema Sepetu, leo Jumatano, Novemba 21, amefika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili ambapo anashtakiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza video za maudhui ya ngono mitandaoni.

 

Wema amefika mahakamani hapo majira ya saa 3 asubuhi akiwa amevaa miwani huku akiongozana na mama yake mzazi, Mariam Sepetu na wakili wa msanii huyo, Reuben Simwanza, na kwenda moja kwa moja hadi kwenye ukumbi wa mahakama hiyo kusubiri kuanza kusikilizwa kwa kesi yake. 

Novemba 1, mwaka huu Wema alipandishwa katika mahakama hiyo akikabiliwa na shtaka la kusambaza video  ya ngono kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, kesi yenye jalada namba KJN/ RB/13607/2018-KUCHAPISHA NA KUSAMBAZA MAUDHUI YA NGONO MTANDAONI.

 

Wema alisomewa shtaka hilo mbele ya Hakimu Mahira Kasonde ambapo alikana kosa hilo kisha kuachiwa kwa dhamana ya Sh. milioni 10 kupitia kwa Salim Limu. Hakimu aliahirishwa kesi hiyo hadi Novemba 20, mwaka huu (jana) ambapo haikusikilizwa kwa sababu ilikuwa Sikukuu ya Maulid.

Hivi karibuni msanii huyo alisambaza mitandaoni video zake za faragha akiwa na mpenzi wake, anayejulikana kama PCK. Licha ya kuomba radhi siku chache baadaye, Bodi ya Filamu nchini ilimfungia msanii huyo kujihusisha na masuala ya sanaa kwa muda usiojulikana huku ikisema adhabu yake halisi inakuja.

 

UPDATES:

Kesi ya Wema Sepetu, ya kusambaza picha chafu mtandaoni imeahirishwa hadi Desemba 12 mwaka huu kutokana na upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.

 

Shauri la kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa katika Maakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya hakimu Maira Kasonde huku upande wa Wakili wa wa utetezi akiwa Ruben Simwanza na upande wa Jamhuri ukisimamiwa na Wakili Jenifer Masue.

Hakimu Kasonde akiiahirisha kesi hiyo amesema kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na akaiahirisha hadi Desemba 12 mwaka huu.

 

Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015, endapo mtuhumiwa atabainika kusambaza picha au video za ngono au zinazoashiria vitendo vya ngono, adhabu ya kosa hilo ni pamoja na faini ya shilingi milioni 20 au kifungo kisichopungua miaka saba jela au vyote kwa pamoja.

WEMA Alivyotinga Mahakamani Tena, Kesi ya Video za Ngono!

Comments are closed.