The House of Favourite Newspapers

Wezi Wapuliza Dawa ya Usingizi, Wawaibia Wafiwa

0

JESHI la Polisi mkoani Pwani wamekamata vifaa mbalimbali vilivyoibiwa katika msiba eneo la Mlandizi, Kibaha mkoani humo.

 

 

Akizungumza jana Alhamisi, Machi 11, 2021, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema vifaa hivyo vimeibiwa baada ya watu wanaodhaniwa kuwa wezi kufika kwenye msiba wa mkazi mmoja wa Mlandizi na kuwapulizia dawa ya usingizi baadhi ya waombolezaji na wafiwa.

 

 

“Watu walikuwa wamekwenda kuzika na wengi walitawanyika, wale wachache waliokuwa wamebaki ilipofika usiku waliingia vyumbani kulala, hawa wezi walipulizia dawa ya usingizi na wafiwa walilala usingizi mzito ikawa rahisi kwao kuvunja kufuli, kuingia ndani na kuiba,” amesema.

 

 

Ametaja baadhi ya vitu vilivyoibiwa ni televisheni na simu za mkononi na kubainisha kuwa katika ufuatiliaji wa tukio hilo watuhumiwa kadhaa wamekamatwa wakiwa na simu mbili na televisheni hiyo, polisi bado wanaendelea kuwasaka wengine.

Leave A Reply