The House of Favourite Newspapers

Winga AS Vita: Mimi, Yanga Mbona Fresh Tu

0

WINGA wa AS Vita, Tuisila Kisinda amesema kuwa asilimia kubwa ya mazungumzo aliyofanya na Yanga yameenda vizuri huku akisema kuwa kilichobaki kwa sasa ni kwa uongozi wa Yanga kumalizia baadhi ya vitu ili akamilishe usajili wake.

 

Winga huyo mwenye umri wa miaka 20 amekuwa kwenye mazungumzo na Yanga kwa muda mrefu na kwa mujibu wa taarifa ilizozipata Championi Ijumaa zinaeleza kuwa winga huyo yupo kwenye mipango ya usajili utakaofanywa na GSM ambao ni wadhamini wa Yanga.

 

Kisinda amesema kuwa amekuwa akizungumza na viongozi wa Yanga kwa muda mrefu na asilimia kubwa ya mazungumzo yamekamilika huku kilichobaki kwa sasa ni kwa upande wa Yanga kukamilisha baadhi ya vitu ambavyo hajaviweka hadharani ili awe mali ya Yanga.

 

“Nimekuwa nikifanya mazungumzo na Yanga kwa muda mrefu, ni kweli wananihitaji na tumekubaliana nao baadhi ya vitu ambavyo kimsingi Yanga wanatakiwa wakivikamilisha tu nakuwa mali yao.

 

“Mimi sitaki kuwa na haraka sana kwa kuwa kila kitu huenda kutokana na wakati wake, kama kweli mambo yataenda sawa nitajiunga na Yanga ambayo nimekuwa nikiifuatilia sana baada ya kuonyesha kuwa wananihitaji,” alisema winga huyo.

 

Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika chanzo chetu cha kuaminika ndani ya Yanga kinasema kuwa Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa GSM na Arafat Haji ambaye ni mjumbe kamati ya utendaji Yanga ndiyo wanasimamia zaidi usajili wa mchezaji huyo.

 

Walipotafuta viongozi hao waligoma kuweka wazi juu ya usajili huo wakidai kuwa muda wa usajili haujafika na pindi utakapokuwa tayari kila kitu wataweka hadharani.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

MREMBO AJITOKEZA KUHAMASISHA WAREMBO KUOLEWA NA WATU WAZIMA WALIOWAZIDI UMRI..

Leave A Reply