The House of Favourite Newspapers

Wolper: Baba P Hanisumbui, Akianza Nitawaambia

0

JACQUELINE Wolper Massawe au Mama P; ni super woman kunako Bongo Movies ambaye amesema kuwa, anamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba, mwanaume aliyenaye kwa sasa ambaye ni mfanyabiashara na mwanamitindo maarufu jijini Dar aitwaye Rich Mitindo.

 

Wawili hao wamejaaliwa mtoto wa kiume waliyempa jina la Paskali ndiyo maana Wolper anajiita Mama P na Rich Mitindo anaitwa Baba P na majina hayo yamekuwa maarufu zaidi kwa sasa.

 

Sasa; baada ya kuibuka maneno mengi kwamba kuna tetesi wanga wamepita na penzi lao, Wolper ametoka hadharani na kuweka mambo sawa akisema jamaa huyo hana tatizo na wako vizuri.

 

Wolper anasema; “Sina matatizo ya Baba P ya kumuelezea mtu kwa sababu inafahamika ni mpole hata kwa mwonekano wake, hanisumbui na akianza kunisumbua nitawaambia…”

 

Leave A Reply