Yajue maajabu ya ndizi mbivu zenye madoa meusi!

ndizoooooBila shaka wengi wetu tunapenda kula ndizi mbivu, lakini ni wachache tunaojua faida zitokanazo na ulaji wa ndizi mbivu zilizoiva sana na kutoa madoa meusi madogomadogo. Leo tutaelezea maajabu yanayoweza kutokea mwilini mwako kwa kula tunda hili lenye ladha tamu na ya kipekee.

Katika utafiti uliofanyika kuhusu tunda la ndizi, imegundulika ukiwa na mazoea ya kula ndizi mbivu mara kwa mara unaweza kuzuia magonjwa kadhaa ukiwemo uvimbe (Tumor Diseases).

Aidha, tafiti hizo zimegundua kuwa ndizi iliyoiva sana hadi kutoa madoa meusi, virutubisho vyake ni bora zaidi kiafya kuliko ndizi iliyoiva kawaida bila kuwa na madoa hayo au iliyoiva na kuwa na rangi ya kijani pekee.

Ikumbukwe kuwa, kadiri ndizi inavyoendelea kuiva, ndivyo virutubisho vyake vinavyozidi kuimarika.

Ndizi ya kuiva ina uwezo mkubwa wa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili (Immunity System), wanga unaopatikana kwenye ndizi mbivu yenye madoa meusi huyeyuka kirahisi inapoingia mwilini na kuwa sukari ambayo ni rahisi kusagika tumboni.

Mtu mzima anashauriwa kula ndizi moja hadi mbili kwa siku ili kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili. Umuhimu wa ndizi mbivu kiafya unatokana na kuwa na kirutubisho adimu kijulikanacho kwa jina la ‘Lentinan’ ambacho kina uwezo wa kuamsha kinga ya mwili na huzuia saratani.

Utafiti uliofanywa na wanasayansi wa Kijapani uligundua pia kuwa ndizi iliyoiva sana huzalisha kitu kijulikanacho kama TNF (Tumor Necrosis Factor) ambacho huzuia utokeaji wa chembe hai zisizo za kawaida na kina uwezo wa kudhibiti mwilini chembe hai za saratani. Mbali ya hayo, kirutubisho hicho huongeza idadi ya seli za damu nyeupe na kwa kiwango kikubwa huimarisha kinga ya mwili.

Kwa kumalizia, napenda kusema kwamba ndizi mbivu zina faida nyingi muhimu kiafya. Ndizi ina uwezo wa kuzuia saratani ambayo inasumbua mamilioni ya watu duniani na faida zingine ambazo ni msingi wa ustawi wa afya ya binadamu. Kula ndizi kila siku ili kulinda afya yako.

Hivyo, ili kuzipata faida za ndizi iliyoiva, hakikisha una ila wakati ule ule inapotoa madoa ili isipoteze virutubisho vyake au baada ya kutoa madoa hayo meusi, unaweza kuiweka kwenye jokofu kuilinda isiharibike. Ila kamwe usiiweke ndizi kwenye jokofu kama haijafikia kiwango chake cha mwisho cha kuiva.


Loading...

Toa comment