The House of Favourite Newspapers

Yanga Hakuna Kuremba, Sarpong na Ulimwengu Kutua

0

HESABU za vigogo wa Yanga ni kumaliza msimu huu kwanza, kisha fasta kuwaingiza mastaa wao wote kambini kuuwinda msimu ujao ambapo wamepania kubeba makombe yote ya ndani.

 

Yanga wanataka kuanza maandalizi ya msimu ujao mapema ili kujenga timu imara kwa kuwaunganisha kiuchezaji mastaa waliokuwepo na wale watakaowasajili.

 

Klabu hiyo ambayo inatajwa kumalizana na nyota kadhaa akiwemo Michael Sarpong na Jules Ulimwengu, wanataka kuwafanya wawe na makali zaidi na nyota watakaowakuta kikosini hapo akiwemo Bernard Morrison, hivyo wamepanga kuwaleta fasta kambini Dar.

Habari za uhakika ambazo Spoti Xtra, limezipata ni kuwa kambi hiyo itaanza mara moja baada ya msimu huu kumalizika.

 

“Kilichopo mbele kwa sasa ni kuona kikosi kinaendelea kuwepo pamoja ambapo baada ya ligi kuisha tu kinachofata ni wachezaji wote kuingia kambini kuanza maandalizi ya msimu ujao.

 

 

“Kambi hiyo itawahusisha wachezaji wote hata wale kina Ulimwengu na Sarpong, ambapo lengo ni kuona tunaunda kikosi ambacho kitakuwa na muunganiko mzuri kwa wachezaji wapya na waliopo.

 

“Hatutakuwa na muda wa likizo kwa wachezaji kwa sababu tayari wamepumzika katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama, kwa hiyo kitakachofanyika ni kuwa wakimaliza tu ligi watajiandaa kwenda kambini,” kilisema chanzo hicho

MORRISON Afanya MAZOEZI Akiwa AMEVAA BARAKOA Mwanzo MWISHO, YANGA Mambo ni MOTO!

Leave A Reply