The House of Favourite Newspapers

Yanga, Morrison Picha Limeanza Upya

0
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela.

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema kuwa unasubiria nakala ya hukumu kutoka kwenye Kamati ya Maadili, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya maamuzi yaliyotolewa kwa kiungo mshambuliaji Mghana, Bernard Morrison kabla ya kwenda ngazi ya juu zaidi.

 

Juzi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Elias Mwanjala alimtangaza Morrison kushinda kesi hiyo kuhusu sakata la kudaiwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga kuwa na kasoro kisha baadaye kumpa nafasi ya kuchagua timu ya kuichezea kwa ajili ya msimu ujao.

Wakati Mghana huyo akishinda kesi hiyo, ameamuliwa kurejesha fedha za Yanga alizozichukua ambazo ni dola 25,000 (zaidi ya Sh 58Mil) huku akipelekwa kwenye Kamati ya Maadili ya TFF kutokana na kosa la kusaini mkataba Simba akiwa kwenye kesi hiyo.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amesema kuwa kamwe hawatabadili maamuzi waliyoyatoa ya kwenda kushtaki kwenye Mahakama ya Usuluhishi ya Kimichezo ya Kimataifa (CAS) pamoja na Fifa.Mwakalebela amesema kuwa mara baada ya kupata nakala ya hukumu, haraka wataanza taratibu za kwenda CAS kwa ajili ya kupinga maamuzi hayo yaliyotolewa na TFF.

Aliongeza kuwa mapungufu ambayo yametolewa na kamati hiyo ya TFF hayapo katika mkataba wao, labda kama wanayo mengine mapya ambayo hawayajui.

 

“Tunasubiri nakala ya hukumu, ili tukate rufaa CAS, kwani bila nakala hiyo CAS hawatatupokea, hivyo ili tupokewe ni lazima tuipate nakala hiyo ya hukumu ambayo ninaamini ndani ya siku hizi mbili tutaipata.

 

“Kama uongozi tumeshangaa na mapungufu wanayoyataja kamati hiyo ambayo hayapo katika mkataba labda kama wanao mwingine. Mkataba tulioutoa mbele ya kamati hauna hayo mapungufu,” alisema Mwakalebela.Mwanasheria wa Yanga, Alex Mgongolwa baada ya hukumu hiyo jana alisikika akisema: “Katika mkataba ni jambo la kawaida kutokea utofauti wa tarehe, hivyo tarehe haiwezi kufanya mkataba kuwa batili.

 

Je aliwezaje kupokea pesa bila kuwa na mkataba!”Katika hatua nyingine Mwekezaji wa Simba, Bilionea Mohammed Dewji ‘Mo’, jana kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii alimkaribisha kiungo huyo na kumpa onyo kwa kumwambia:“Karibu Simba, Bernard Morrison. Tunaamini utakuja kuwa sehemu ya kuendeleza na kukuza misingi tuliyojiwekea ya nidhamu, kujituma na kujali maslahi ya klabu kwa jumla.”

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Leave A Reply