The House of Favourite Newspapers

Yanga msiogope APR hawapiti kwa Bossou

0

APR

Wachezaji wa APR wakishangilia.

Na Mohammed Mdose
KIUNGO wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema ni kazi rahisi kuimaliza APR katika mechi ya marudiano leo ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kusonga mbele kwani kubwa walishaifanya awali.
Katika mchezo wa kwanza wikiendi iliyopita mjini Kigali, Rwanda, Yanga ilishinda mabao 2-1 yaliyofungwa na Juma Abdul na Thabani Kamusoko huku lile la APR likifungwa na Patrick Sibomana.

NIYONZIMA (7)

Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima.

Leo timu hizo zinarudiana kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo na timu itakayovuka itacheza na Al Ahly ya Misri au Recreativo do Libolo ya Angola.
Niyonzima aliliambia Championi Jumamosi kuwa, ushindi wa kwanza ni chachu ya kufanya vizuri leo, hivyo APR aliyowahi kuichezea kabla ya kujiunga na Yanga, ijiandae kwa kipigo kingine.
“APR ni timu nzuri na walifanikiwa kutuzuia kwa kiasi katika mchezo wa kwanza, lakini hiyo haimaanishi kuwa tutakaporudiana watatusumbua tena, Yanga ni nzuri zaidi ikicheza nyumbani.
“Kwa sasa akili zetu zote zinawaza mchezo huu ambao nataka kuwahakikishia mashabaki wetu kuwa lazima tuwafunge tena APR na hata wao walijue hilo kuwa tutawafunga tena,” alisema Niyonzima.

Leave A Reply