Yanga SC yafunika mapokezi Songea

MAELFU ya mashabiki wa Yanga jana walifurika kupokea msafara wa timu hiyo uliofika saa sita mchana kwa ajili ya mchezo wa dhidi ya KMC FC.

Timu hizo zitavaana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa kesho Jumanne saa kumi kamili kwenye Uwanja wa Majimaji Songea.

Katika mchezo huo, Yanga watakuwa watakaribishwa na KMC ambao wamechagua kuutumia uwanja huo kama wa nyumbani kwa mujibu wa sheria za ligi zinazoruhusu kupeleka mechi mbili kwenye uwanja mwingine.

Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa timu hiyo, Hafidh Saleh alisema kuwa msafara huo ulifika saa sita mchana na kupokelewa na maelfu ya mashabiki kwa kuanzia Uwanja wa Ndege wa mkoa.

Saleh alisema kuwa baada ya kupokelewa hapo, msafara wa timu hiyo ulielekea hotelini ukisindikizwa na maelfu ya mashabiki hao waliosababisha barabara na mitaa kufungwa ili kupisha msafara huo.

“Tunashukuru tumefika salama Songea, lakini tumekutana na saprazi ya rundo kubwa la mashabiki waliotupokea kwa kuanzia Uwanja wa Ndege hadi hotelini waliotusindikiza kwa kutumia miguu, magari na bodaboda zilizokuwa zikiongoza msafara kuanzia eapoti,”alisema Saleh.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam2178
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment