The House of Favourite Newspapers

Diamond na Harmonize Wajibizana Kwa Vitendo

0

Hakuna muda wa maneno mengi, bali kinachoendelea ni majibizano ya kivitendo zaidi kati ya Diamond Platnumz na Harmonize; mmoja akifanya shoo ya kibabe, mwingine analipiza kwa shoo ya kibabe.

Mfano; wikiendi iliyopita, baada ya Diamond kufanya shoo yenye ujazo pande za Minneapolis, Harmonize au Konde Boy Mjeshi alimjibu kwa shoo baab’kubwa huko Boise, Idaho nchini Marekani.

Kwenye shoo zote hizo, kila mmoja alionesha umwamba wake kutokana na nyomi kubwa lililojitokeza na kushuhudia kila mmoja akikata kiu ya mashabiki wake.

Kwa Diamond ilikuwa ni shoo ya tatu, lakini kwa Harmonize tayari amefanya shoo kubwa zaidi ya tano nchini humo.
Nje ya shoo, pia jamaa hao wamekuwa wakijibizana kwa vitendo kwani baada ya Harmonize kununua cheni moja matata inayowakawaka, Diamond amemjibu kwa kununua saa aina ya Rolex ya shilingi milioni 69.

Pia kuna kofia ya raundi ambayo Diamond amekuwa akiivaa, nayo tumeshuhudia Harmonize akiitafuta na kuonekana nayo. Pia kuna koti moja la kinyamwezi alionekana nalo Harmonize ambalo Diamond naye ameonekana nalo na kuibua mjadala kama wote.

Cc; @sifaelpaul

Leave A Reply