The House of Favourite Newspapers

Esma Anapiga tu Pesa

0

ESMA Khan almaarufu Esma Platnuzm ni dada wa supastaa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul au Diamond Platnumz ambaye amefunguka namna anavyopiga pesa ndefu kwenye biashara kutokana na namna alivyo bahili.

 

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Esma anasema kuwa, mtu anapokuwa ni staa na akashindwa kudhibiti pesa anazozipata kwa kuendekeza starehe, lazima atafunga biashara mapema.

 

Amesema kwa upande wake amekuwa ni bahili kupitiliza kiasi kwamba mpaka watu wanamshangaa.

“Kwenye biashara kama siyo ubahili huwezi kuendelea hata kidogo, tena kwa sisi wenye majina ndiyo hatari kwa sababu tunapenda sana starehe hivyo ni muhimu kuweka ubahili mbele na ndiyo maana watu wananishangaa,” anasema Esma ambaye amekuwa akishambuliwa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tabia ya kuwageuka mawifi zake akipewa jina la Yuda Iskarioti.

STORI; IMELDA MTEMA, DAR

Leave A Reply