The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tuko Fiti Kinona… Tambwe, Ngoma Warejea… Zanaco Wataisoma Namba

KIKOSI cha Yanga kimeendelea kujinoa ili kujiiimarisha vyema kwenye mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Zanaco ya Zambia, mchezo wa Ligi ya Klabu Bingwa Barani Afrika.
 
Mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma aliyekuwa na msuguano kiainana uongozi wa klabu yake ameanza mazoezi katika kikosi hicho.
Ngoma ameanza mazoezi baada ya siku kadhaa za kuidengulia timu hiyo kwa kisingizio cha kuumwa.
Hata hivyo, baadaye iligundulika ilikuwa ni janja, jambo ambalo liliwaudhi Wanayanga wengi.
Wakati Ngoma anaanza mazoezi, Amissi Tambwe ambaye alikuwa majeruhi na kufikia hadi kung’ang’ania kucheza, naye amerejea mazoezini.
Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa, amesema wachezaji hao tayari wameanza kujifua na wenzao.
“Tayari wako mazoezini lakini suala la kucheza Jumamosi kwa kweli sijui, au ni niseme wana asilimia chache sana,” alisema.

PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.