The House of Favourite Newspapers

Yanga: Tunachukua Tena Kombe la ASFC… leo Jumapili Kuvaana na Rhino Rangers

0

WAKIWA wanashuka uwanjani leo Jumapili kuvaana na Rhino Rangers ya Tabora katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC), mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Yanga wamesema watahakikisha wanashinda mchezo huo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutimiza malengo yao ya kutetea taji lao.

Leo Jumapili kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar, Yanga wanatarajiwa kuwa wenyeji wa Rhino Rangers katika mchezo wa raundi ya tatu ya mashindano hayo.

Yanga wanatarajiwa kuingia katika mchezo huo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Kurugenzi katika raundi ya pili ya mashindano hao, huku wakiwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo baada ya kubeba ubingwa msimu uliopita mbele ya Coastal Union.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Tunatarajia mchezo wa ushindani kutokana na ukweli kwamba wapinzani wetu wana tufahamu zaidi kulinganisha na sisi tunavyowafahamu, lakini pia kwa kuwa huu ni mchezo wa hatua ya mtoano ambao ukipoteza basi umeondoshwa kwenye mashindano, hivyo timu nyingi hukamia.

“Tunajivunia maandalizi bora ambayo tumeyafanya, kama mabingwa watetezi malengo yetu ni kushinda mchezo huu ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wetu.”

STORI NA JOEL THOMAS

Leave A Reply