The House of Favourite Newspapers

Yanga Yabadili Majukumu ya Kotei Simba

0

Na Wilbert Molandi
KOCHA Msaidizi wa Simba, Mganda, Jackson Mayanja, ametaja sababu ya kumchezesha nafasi ya beki wa kati Mghana, James Kotei ni baada ya kucheza kwa kiwango kikubwa kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga mwishoni mwa Februari, mwaka huu.
Kauli hiyo, aliitoa juzi Jumamosi mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Azam FC ambayo Simba ilishinda 1-0 lililofungwa na Mohammed Ibrahim ‘Mo’.
Katika mechi hiyo ya Azam, Kotei alicheza namba 5 kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Yanga ambayo alianza kwa kucheza 6 kabla ya kurudishwa nyuma baada ya beki, Besala Bokungu kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Mayanja alisema wamelazimika kumbadilishia majukumu kutokana na kutokuwepo kwa mabeki wao wa kati, Novalty Lufunga aliye majeruhi na Abdi Banda ambaye hana fitinesi ya kutosha, hivyo wakalazimika kumtumia Kotei katika nafasi hiyo kwa kutambua kiwango alichokionyesha dhidi ya Yanga.
“Sababu kubwa iliyotufanya tumpange Kotei kucheza beki wa kati, badala ya kiungo mkabaji ni kiwango kikubwa alichokionyesha kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Yanga.
“Katika mechi hiyo, Kotei alijitahidi kuzuia na kuokoa hatari golini kwetu timu ikiwa pungufu baada ya Bokungu kupewa kadi nyekundu katikati ya mchezo huo.
“Hivyo, tukaona leo (juzi) mechi na Azam tumpange kucheza nafasi hiyo, ni baada ya mabeki wetu Banda na Lufunga kutokuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo,” alisema Mayanja.

Leave A Reply