The House of Favourite Newspapers

Yanga Yaifunga Kagera Sugar Bao 2-1 Kaitaba

TIMU  ya Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar leo katika  Uwanja wa Kaitaba, Bukoba. Mabao kwa upande wa Yanga yamefungwa na Heritier Makambo dakika ya 21  kipindi cha kwanza na Raphael Daudi dakika ya 74 kipindi cha pili na bao la Kagera Sugar limefungwa kwa Penati  na Ramadhani Kapera dakika ya 48 kipindi cha kwanza.

 

Yanga wamefikisha poiti 32 wamecheza michezo 12 na kushika nafasi ya pili nyuma ya Azam FC wenye pointi 33 wakiwa wamecheza michezo 13.  Timu ya Simba inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 27 wakicheza michezo 12.

 

Takwimu za mchezo zinaonesha Kagera Sugar ilipiga mashuti mengi zaidi yaliyolenga goli kuliko Yanga.

Comments are closed.