The House of Favourite Newspapers

Yanga Yapata Vikosi Vitatu Moro

MASHABIKI wa soka bado hawajakiamini kikosi cha Yanga, lakini Mwinyi Zahera amewaambia kwamba kambi ya Morogoro imempa vikosi vitatu ambavyo vinaundwa na mchanganyiko wa wachezaji chipukizi na wakongwe.

 

Kikosi cha kwanza kati ya hivyo ni kile kinachoundwa na kipa, Klaus Kindoki kutoka DR Congo, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Feisal Salum ‘Fai Toto’ Deus Kaseke, Papy Tshishimbi, Mrisho Ngassa, Rafael Daud pamoja na Heritier Makambo.

 

“Ukiachana na kikosi hicho kikosi cha pili kinaweza kuundwa na kipa, Beno Kakolanya, Paul Godfrey, Haji Mwinyi, Pato Ngonyani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ Juma Makapu, Juma Mahadhi, Thaban Kamusoko, Emmanuel Martin, Amisi Tambwe na Ibrahim Ajibu.

“Kikosi cha tatu nilichokipata ni kile kinachoundwa na wachezaji wengi ambao ni chipukizi wakiongozwa kipa, Ramadhan Kabwili, Jafar Mohammed, Mohammed Issa ‘Banka’, Pius Buswita, Maka Edward, Said Mussa, Matheo Anthony, Yusuph Muhilu na kuna wachezaji wengine kama watatu hivi wa kutoka kikosi cha vijana ambao nao ni wazuri,” alisema Zahera.

 

“Kutokana na ubora wa vikosi ndiyo maana najiamini kuwa nitafanya vizuri ligi kuu kwani ikitokea mchezaji mmoja ameumia yupo wa kuziba nafasi yake tena kwa ustadi mkubwa ukizingatia baada ya kuondoka Hassan Kessy wengi walijua kuwa nafasi ya beki wa kulia amebakia Juma Abdul peke yake.

 

“Lakini ukweli ni kwamba, pengo hilo nimefanikiwa kuliziba na sasa nafasi hiyo inawachezaji zaidi ya watano wanaoweza kuicheza vizuri, wawili wanatoka kikosi cha vijana na wengine ni Ninja, Pato lakini pia Mahadhi anaweza kuicheza vizuri nafasi hiyo,” alisema Zahera.

 

Mfumo ambao Zahera amekuwa akitumia mazoezini ni kushambuliana kwa kasi huku pia wachezaji wote wakipigwa marufuku kupiga pasi za nyuma pasipo sababu yoyote ya msingi, pasi ambazo walitakiwa kupiga ni za kwenda mbele tu, jambo ambalo walionekana kulifanya kwa ustadi mkubwa.

BEKI MATATA

Zahera hana hofu hata chembe na safu yake ya ulinzi ambayo inaongozwa na beki mkongwe, Kelvin Yondani ambaye hivi karibuni alipewa unahodha wa Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kustaafu wengine ni Andrew Vicent ‘Dante’, Juma Makapu na Juma Shaibu ‘Ninja’.

 

“Ninajisikia furaha kuona mabadiliko makubwa katika timu yangu kwa kuanzia safu yangu ya ulinzi niliyoitengeneza katika kipindi cha maandalizi tukiwa kambini kwa kuonyesha kiwango kikubwa ambacho kimenipa matumaini ya kufanya vema katika ligi na michuano mengine tutakayoshiriki.

 

“Nimefarijika baada ya mabeki wangu kucheza mechi tatu mfululizo za kirafiki bila ya kuruhusu bao, hicho ndiyo kitu nilichokuwa ninataka kukiona, kwani msingi wa timu unaanzia nyuma golini kwetu.

 

“Nimemuona Dante akiwa na fiziki ya kutosha katika mechi hizi tulizocheza kwa maana si yule niliyemkuta baada ya kumtengeneza vizuri katika fitinesi,” alisema Zahera ambaye makazi yake yapo karibu na Ufukwe wa Bahari ya Hindi maeneo ya Kawe.

 

 

Comments are closed.