The House of Favourite Newspapers

Yatima wamshushia maombi Wema

0

wemaWema Isaac Sepetu ‘Madam’

AStori: Imelda Mtema, Wikienda

DAR ES SALAAM: BAADHI ya watoto yatima kutoka Kituo cha Mitindo House kilichopo Msasani, Dar, wamemshushia maombi mazito mkali wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ huku wakisema kuwa kwa upendo aliowaonesha amethibitisha ni kwa kiasi gani yeye ni mama bora.

WEMAYatima wakimuombea Wema

Juzikati Wema aliwaandalia futari watoto hao waliojumuika katika Mgahawa wa Hadija Mwanamboka uliopo maeneo ya Morocco, Dar ambapo walimfurahia bi dada huyo kwa kuwakumbuka na kufuturu nao kwani muda wote walikaa naye wakipiga stori kabla ya kumwangushia maombi na kumsifia kuwa anajua kuwapa watoto malezi bora.

Kwa upande wake, Wema aliliambia Wikienda: “Nimefarijika sana kujumuika na watoto hawa, kwangu ni faraja kubwa, ninaona nina amani sana ndani ya moyo kwani watoto hawa wanahitaji upendo wa hali ya juu,” alisema Wema. Pamoja na kufuturu nao, Wema aliwapa watoto hao misaada mbalimbali ya vyakula kama mafuta, mchele, sabuni na vitu vingine kwa ajili ya mahitaji ya kila siku.

Leave A Reply