The House of Favourite Newspapers

Yondani Kuanza Na Bosi Wake Lwandamina

0

 

KELVIN Yondani, ingizo jipya ndani ya kikosi cha Polisi Tanzania kesho anatarajiwa kuanza kazi dhidi ya bosi wake wa zamani kwenye benchi la ufundi George Lwandamina ambaye anaifundisha Azam FC.

 

Lwandamina mwenye miaka 57 raia wa Zambia, alimfundisha Yondani alipokuwa kocha wa Yanga msimu wa 2016/18 hivyo kesho anakutana na mwanafunzi wake akiwa kwenye maskani mapya.

Yondani amejiunga na Polisi Tanzania kwa dili la mwaka mmoja akiwa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na timu yake ya Yanga kumeguka msimu wa 2019/20 na hakuongeza mkataba mwingine.

 

Akizungumza na Championi Jumatano,Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro alisema kuwa taratibu zote kuhusu usajili wa Yondani zimekamilika.“Uongozi umekamilisha kila kitu kuhusu mchezaji wetu Yondani hivyo kwa sasa ni kazi ya benchi la ufundi kuamua kama atamtumia ama la, ila sisi hatuna tatizo naye,” alisema Lukwaro.

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam

Leave A Reply