The House of Favourite Newspapers

Young Thug Abadili Jina, Sasa Kuitwa ‘No, My Name Is Jeffery’

0

young-thug-denimRAPA maarufu duniani kutoka kiwanda cha Hip Hop, Young Thug ametangaza kubadili jina lake hilo. Taarifa zilizotolewa na Kiongozi Mkuu wa Lebo ya 300 Entertainment, anayofanya kazi, Lyor Cohen, staa kwa sasa ataitwa kwa jina jipya la: No, My Name Is Jeffery.

Cohen amesema kuwa, uamuzi huo wa Thug umekuja ikiwa ni moja ya  mapinduzi katika kazi zake ambayo yanakuja na mixtape yake mpya iliyoko kwenye hatua za mwisho za maandalizi na ataichia hivi karibuni ambayo ameipa jina la  Jeffery.

“Young Thug hatakuwa Young Thug tena,” Cohen alisema. “Jina lake jipya ataitwa No, My Name Is Jeffery. No, My Name Is Jeffery. Hilo ndilo jina lake jipya. Na ukweli ni kwamba, ukiona hivi utambue kuwa ni biashara… Hatuna budi sote kulikubali jina la Jeffery ili kusapoti kile anachokifanya zaidi na zaidi.”

thugMapema juzi, Thugger aliachia list ya mastaa waliyomo kwenye mixtape yake ya Jeffery ambamo ndani yake amewashirikisha mastaa kibao wakiwemo Elton John, Birdman, producer Swizz Beatz, na mwanamasumbwi Floyd Mayweather.

Jeffery alifanya sherehe ya birthday ya kutimiza miaka 25 ya azaliwe.

Leave A Reply