The House of Favourite Newspapers

Zari Awatupia Dongo Wanaodanga, Amkumbuka Mumewe

Mfanyabiashara Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ akiwa na aliyekuwa baba watoto wake marehemu, Ivan Ssemwanga kabla hawajawa matajiri.

 

MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ jana ameandika ujumbe wa kumkumbuka aliyekuwa baba watoto wake, Ivan Ssemwanga aliyetimiza mwaka mmoja toka afariki.

Jana ametumia akaunti yake ya Instagram kuandika ujumbe kwa kina dada wanaodanga wakidhani watawapata wanaume wakaobadilisha maisha yao, kitu ambacho kwa upande wake amekiita ni kama kurusha jiwe gizani kwa kuwa wanatakiwa kutafuta mtu ambaye wataishi naye na kubadilisha maisha yao kama alivyofanya kwa Ivan enzi za uhai wake ambapo alimkuta bado hajawa tajiri.

Zarina akiwa ‘outing’ na Ivan.

Mrembo huyo ambaye pia amezaa watoto wawili na muimbaji Naseeb Abdul  ‘Diamond Platnumz’, amepost picha mbalimbali za zamani akiwa na marehemu Ivan na kuandika ujumbe wa maneno mbalimbali.

Hapa chini ni ujumbe aliou-post Zari kwenye akaunti yake.

Pale unaposikia pesa za urithi hapo vipi. Success isnt sexually transmitted my dear. Endeleeni kudanga thinking some rich guy will knock you off your feet and success will happen over night.,” aliandika Zari kupitia Instagram.

Aliongeza, “Even if he did you will be like part of the furniture he has a right to take out old ones and bring in new ones, as for me its not easy to get rid of me. IAM THE FOUNDATION not the roof…haha. anyway we are commemorating Ivans one year since his passing and i thought I’d motivate someone out there with these old images. Dont downlook broke guys, God is for all, tables turn! Poor thing worked day and night to get me this car at 22 because he saw the woman in me. And yes, it didnt work out no matter how much i tried, Started from the bottom, right! Rest his soul in peace!,”

Mashabiki wake wamekuwa wakitoa maoni katika picha hizo kwa kusema kuwa ametoa dongo hilo la kudanga kuelekea kwa mastaa wa Bongo, Hamisa Mobeto na Wema Sepetu ambao wamekuwa wakimfuatilia Diamond na kusababishia agombane na kuachana na mwanamuziki huyo.

Comments are closed.