The House of Favourite Newspapers

Zitto, Nay wa Mitego Walaani R.O.M.A Kuvamiwa na Kukamatwa na Polisi Usiku

IKIWA ni saa chache baada ya Mbunge wa Mikumi na staa Bongo Fleva Joseph Haule ‘Prof Jay’ kutoa taarifa kupitia account yake ya Instagram kuhusu kukamatwa kwa staa mwingine wa Hip Hop Roma Mkatoliki katika studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana, taarifa hiyo imeamsha hisia za watu mbalimbali wakiwepo mastaa wa Bongo Fleva na wanasiasa.

Leo April 6 2017 kupitia account zao za Instgram na Twitter Rapa Nay wa Mitego na Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe wameyaandika.

 

Naye Rapa Nay wa Mitego ameandika

Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?!  Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.” – Nay wa Mitego.

 

Comments are closed.