The House of Favourite Newspapers

Zuchu Amjibu Kibabe Bosi Wake Diamond Kulipa Bil.10 Aondoke Wasafi

0
Malkia mpya wa muziki wa Kizazi Kipya nchini TanzaniaZuhura Othman almaarufu Zuchu.

 

Zuhura Othman almaarufu Zuchu; ni malkia mpya wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania ambaye amejibu kauli ya bosi wake pale Wasafi, Diamond Platnumz kwamba siku akitaka kuondoka kwenye lebo hiyo basi atalipa shilingi bilioni 10 ili kuvunja mkataba.

 

Zuchu anasema kuwa, hana shida kulipa kiasi hicho cha pesa kama atataka kuondoka Lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond.

 

Diamond alitoa kauli hiyo alipokuwa akimjibu shabiki aliyemuuliza Zuchu atalazimika kulipa kiasi gani cha pesa ili aondoke Wasafi?

Bosi wa Wasafi, Diamond Platnumz

“Aahh huyo si chini ya 10 Bilioni, si unaona manamba yake huko mjini YouTube baba…” Alijibu Diamond.

Wakati Zuchu akijibu matamshi ya bosi wake huyo anasema; “Msanii anapoamua kubaki au kuondoka kwenye lebo naamini kila mkataba una makubaliano yanayopendelea pande zote mbili; ulikaa na kukubaliana, ikiwa ni shimo uliloingia ulichimba hela mwenyewe.

 

“Ikiwa kuna mambo ulitaka yabadilishwe ulikuwa na nafasi ya kufanya hivyo mwenyewe. Kila kitu kinajadiliwa, wasanii walikuwa wanaondoka WCB hata kabla sijajiunga, kama ingetegemea mambo mengine ningesaini mkataba.”

 

Hata hivyo, wapo wanaosema kuwa, Diamond hakumaanisha kile alichojibu bali ilikuwa ni katika hali ya utani tu, japokuwa kuna wanaosema alimaanisha kile alichokisema kutokana na mapato makubwa anayoyapata kutoka kwa Zuchu hivyo hayupo tayari kumuachia aondoke kirahisi.

STORI NA SIFAEL PAUL | GAZETI LA IJUAA

MREMBO ALIYETUPWA JELA SAUZI AFRIKA MIEZI 6, BAADA YA KUGOMA KUUZA MWILI KWA BOSS | MAPITO..

Leave A Reply