The House of Favourite Newspapers

Davido Ammwagia Sifa Baba’ke Kwa Kufadhili Wanafunzi

0

davido-2MWANAMUZIKI Davido wa Nigeria, amemmwagia sifa kedekede baba yake kwa kufadhili masomo ya chuo kikuu kwa wanafunzi wapatao 100 ambao walihitimu jana katika Chuo Kikuu cha Adeleke ambacho kiko chini ya umiliki wake.

Davido, ambaye mashabiki wake humwita Omo Baba Olowo, amefurahishwa sana na hatua hiyo ya baba yake ya kuongeza ustawi wa jamii nchini humo kwa kutoa elimu ya bure kwa watu wanaoitaka, jambo ambalo alisema iwapo lingeigwa na watu wengi Nigeria ingepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Akitupia katika mtandao aliandika: “Ninampenda sana baba yangu kwa kuwasomesha wanafunzi zaidi ya 200 ambapo nusu yao wamesoma kwa ufadhili wake!!!  Mungu akubariki kwa niaba yetu sote, baba!!!  Ninakupenda sana!!!”

Leave A Reply