The House of Favourite Newspapers

Kambi ya Lowassa yamfungukia Wolper

0

WOLPER (5)    Jacqueline Wolper akitangaza kuhamia CCM.

Na Ojuku Abraham, RISASI mchanganyiko

DAR ES SALAAM: Kambi ya aliyekuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa imemfungukia muigizaji wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper, siku chache tu baada ya kutangaza kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) mjini Dodoma.

WOLPER (4)Wakizungumza na Risasi Mchanganyiko kwa nyakati tofauti juzi jijini Dar es Salaam, wasemaji wa kambi hiyo walisema alichokifanya Wolper ni utashi wake wa kisiasa, unatokana na hisia zake, ingawa pia walimsema kama mtu asiyefahamu misingi, sera, itikadi, imani wa ilani za Chadema.

WOLPER (3)Msemaji binafsi wa Lowasa, Aboubakary Liongo, aliliambia gazeti hili kuwa ni vigumu kwa kiongozi huyo kumzungumzia Wolper kwa sababu hakukuwahi kuwa na ‘connection’ ya moja kwa moja baina yao, isipokuwa msanii huyo alijiunga na wanamabadiliko kwa utashi wake mwenyewe.

“Mzee hawezi kumzungumzia, alikuja huku kama ambavyo vijana wengine wengi walikuja wakifuata mabadiliko, kama kuna wa kumzungumzia, labda ni viongozi wa chama kwa sababu operesheni zote zilizokuwa zikifanywa wakati ule, ziliratibiwa na chama.

WOLPER (1)“Wao ndiyo wanaweza kuwa na la kusema kuhusu yeye, ila ninachokiona mimi ni kuwa Wolper ni mtu mzima, mwenye akili timamu, alikuja kwa utashi wake na kama anaondoka, pia anafanya hivyo kwa utashi wake,” alisema Liongo, ambaye ni mtangazaji mwandamizi wa redio nchini.

Kwa upande wake, msemaji wa Chadema,  Tumaini Makene, alisema Wolper ni mtu asiye na msimamo, asiyeelewa misingi, ilani, sera wala itikadi za Chadema, ndiyo maana haelewi nini anafanya.

WOLPER-GWANDA.jpg“Sisi tuko na watu wanaoishi kwa matendo, siasa ni maisha ya binadamu, mtu ‘siriaz’ anajua misingi, itikadi, falsafa, imani na ilani za chama chake, hawezi kuwa leo anaamini hivi kesho vile, ukiona mtu kama huyo, ujue hana msimamo, anayumbishwa na ni mtu anayefuata mkumbo,” alisema Makene.

Lowassa 2Aliyekuwa Mgombea Urais wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kwa tiketi ya Chadema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowasa

Msemaji huyo alitolea mfano wa vyama viwili vikubwa vya siasa nchini Marekani, Republican na Democrat, akidai waumini wa taasisi hizo mbili za kisiasa, ni watu wenye weledi wanaojua nini wanafuata, hivyo siyo rahisi kuona mtu akihama ovyo kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Wolper ambaye aliwahi kuwasuta waigizaji wenzake walioamua kujiunga na CCM kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, akisema ni watu wasioitakia mema taifa kwa kushindwa kuungana ili kulikomboa, hivi karibuni alitangaza kurejea chama tawala, akisema anarudi nyumbani kwani alipotea njia.

“Nimerudi na sifikiri tena kugeuka nyuma, nimeona jinsi rais wetu anavyopigana na chama hiki kuwakomboa wanyonge na sasa hivi kina kasi ya ajabu na nitaendeleza niliyoyaacha,” alisema msanii huyo wakati wa hafla ya kumuaga Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete mjini Dodoma.

Leave A Reply