The House of Favourite Newspapers

Oya mwana… ukizoea kupanda punda, farasi huwezi!

0

Masela inakuwa nini watu wa Saa Godi? Ebana kwenye kitu cha mwezi dume nimejifunza mambo kichizi kutoka kwa makachala. Ilikuwa noma sana aisee arifu kozi pipo walikuwa hawatokei kijiweni au ubaoni kabisa mazee. Bati Mungu mkubwa kozi hatimaye mambo yamekuwa kwenye levo ageini.

Kama vipi acha turudi kwenye mastori moo yanayowazingua masela dheni tuone kama yaliyomo yamo? Basi barida arifu kaa mkao wa kula.

Huku na huku mtu mzima niko apeche alolo bati kama kawa si ndo nikakutana na ishu moko fekelo kinoma? Haikuwa freshi hata kidogo mazee. Bifoo sijanyaka mchongo freshi wa nini kinahapeni, nilidhani wana wanafanya masihara hadi niliposhuhudia ngumi chuma na chupa zikirushwa kama mvua daadeki.

Baba la baba nikaona isiwe kitu, nikazama mzigoni kama kawiz kufaindi sosi ya vita ambayo ilionekana dhahiri kichwa kinaweza kulosti kitu cha pumzi kidandaradandara wanangu.

Si ndo wanoko wa ishu za watu wakaning’ata sikio? Eti mazee sosi ya vita ilikuwa ni shosti ambaye ni baamedi alikuwa amewazingua masela.

Unaambiwa jamaa walikuwa wakimsarendea baamedi mmoko mkare, kitu waiti, mbebiz kaenda hewani sekunde kiasi kwamba hata kaka mkubwa nilipompiga chabo, nikajikuta nazima fegi.

Wana wakanitonya kuwa wale washkaji zangu waliokuwa wamelianzisha, mmoko ndo alikuwa anamuweka mkiksi tauni dheni msela mwingine akataka ale tu wepesi bila kugharamia. Inakuwaje sasa mtu mzima unataka vya watu kimbululambulula bila kujua kuna mmiliki?

Nilitaka kujua kama msela aliyetaka vya watu alikuwa anajua ni shori wa msela, nikaambiwa alikuwa ananyaka mchongo eituzedi bati akawa anasebenza kwa sekreti.

Oya masela, kwenye taimu tuliyonayo asikudanganye kichwa, hakuna sekreti. Siri si ndo ikavuja? Unaambiwa mabaamedi wenzake wakaona wivu mwenzao anapiga bao, wakaamua kubumburua mambo kwa mwenye mali kuwa anaibiwa.

Dah! Mwana akaona kama Rich Mavoko alizingua vile kusema eti mali zako zinachukuliwa dheni wewe unasema ni siri ya ndani! Akaamua kulisanua ili apatikane wina ijulikane moja.

Mazee kama nilivyosema bifoo ilikuwa kama masihara vile, njemba mwizi alipotinga kaunta na kuagiza maunywaji si ndo akashangaa anapokea makonde kama ya Francis Cheka?

Hapo ndo ulipoibuka mtiti wa kilo bee arifu. Huku ngumi kule chupa unaambiwa ilikuwa ni fulu kwere chaliiangu. Mazee unaambiwa kama umezoea kupanda punda dheni farasi huwezi kozi ngumi zilipigwa hadi wana wakawaamulia na sasa kila mmoko anasikilizia maumivu.

Mmenisoma wana? Mambo ya kugombea mashori ni ya kiloko kinoma kozi mbona masistaduu wapo wa kumwaga? Kama vepe sii yuu neksti wiki.

Leave A Reply