The House of Favourite Newspapers

Steve Nyerere Awatolea Uvivu Viongozi Wanaopinga Chanjo “Wanaowashwa Watakunwa” – Video

0

MWENYEKITI wa Jukwaa la Mama Ongea na Mwanao ambaye pia ni balozi wa kuhimiza Chanjo ya Corona, Msanii Stevene Mengere maarufu kama Steve Nyerere amewatolea uvivu baadhi ya viongozi walioko madarakani na wastaafu wanaopinga chanjo ya corona na kuwarubuni wananchi wasichanjwe akisema kuwa wanawashwa hivyo watakunwa.

 

Nyerere amesema hayo leo Ijumaa, Agosti 13, 2021 wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

 

“Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alianza yeye kuwa mfano wa kuigwa wa kuchanjwa. Asingeanza yeye akachanja Muhogo Mchungu kila mtu angesema yake, lakini aliyeanza kuchanja ni Amiri Jeshi Mkuu, akafuata Waziri Mkuu, vyombo vya Ulinzi na Usalama na akasema kuchanja ni hiari.

Hakuna mtu ambaye anafuatwa nyumbani anaambiwa unachanja au huchaji? Matokeo ya vifo unayoyaona wewe mwenyewe unasema mimi nisichanje ni nani? Maamuzi ni hiari unayo mwenyewe rohoni mwako kibinadamu na una haki ya kuchanja au kutokuchanja.

Sisi kama #Uzalendo tunasema kuchanja ni hiari lakini kwa ajili ya maisha yako kachanje, wapo watu wameshachanja huko majuu lakini wanatumika kisiasa kuhimiza wenzao wasichanje, kama hutaki kuchanja nyamaza, tulia, waache watu watumie uhuru wao.

Kama rais wetu kachanja na ndiye kiongopzi mkuu wa Serikali, wewe ni nani? na umepewa uhuru wa kuchanja ama kutochanja, sisi tumeamua kuchanja na tunahimiza wale wanaowashwa kuwahimiza Watanzania wasichanje, watakunywa, maana ukiwashwa lazima ukunwe.

“Kwa wale wastaafu waliokuwa na dhamana kubwa katika nchi hii, kama hawataki kuchanja wanyamaze, tusitumie mitandao kana kwamba wewe ndio una uwezo wa kuandika sana na kuyajua mambo.

 

“Wengine wanaenda mbali kabisa kwenye uroho wa madaraka, nahimiza hadharani ifike wakati ilinde heshima yako, uliitafuta na ulikuwa na dhamana kubwa katika Taifa, acha Watanzania wachanje.

 

“Rais Samia amesema hakuna mchakato mwingine zaidi ya kujenga nchi na kuinua uchumi wetu, ndiyo focus yake, mambo ya Katiba Mpya hayo yenu, vijana wengi ‘wanalishwa sumu’ sijui fanya hivi na hivi, lakini wanaoumia ni wao, ukilishwa ukatoka nayo sio wa leo wewe.

“Natoa tamko, vijana tusilishwe maneno au vitu ambavyo hatuviwezi, twendeni na sera moja tu ya kushirikiana na Serikali kuinua uchumi wetu. Mungu aliibariki Tanzania kwa amani, utulivu na mshikamano, msilishwe embe ng’ong’o ukadhani ni tamu, mwisho lina mwiba.

“Viongozi wanaotumika kisiasa kutaka kutuvuruga sisi wananchi tunasema ukiwasha utakunwa na wakunaji wapo. Kikubwa twendeni tukachanje, hasara ya kuchanja si ya Mhe. Rais, ni ya mimi na wewe, wanaopinga chanjo tuwapuuze,” amesmea Nyerere.

 

Leave A Reply