The House of Favourite Newspapers

Azam FC Yatangaza Viingilio vya Mechi yao na Mbabane

 

Ofisa Habari wa timu hiyo, Jaffar Idd akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).

TIMU ya Azam, imetangaza viingilio vya mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland utakaopigwa Jumapili ijayo kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, amesema mchezo huo utakaoanza saa 1:15 usiku, kiingilio cha chini kitakuwa ni Sh 3,000 kwa mzunguko, V.I.P B Sh 5,000 na V.I.P A Sh 10,000.

“Tumelazimika kuweka kiwango hicho ambacho ni cha kawaida ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kuja kutoa sapoti kwa wawakilishi hawa wa Tanzania.

“Tiketi zitaanza kuuzwa kesho Jumatano ambapo safari hii zitatumika tiketi za elektroniki tofauti na ilivyozoeleka kwenye michezo ya ligi kuu ambapo huwa tunatumia tiketi za kawaida katika uwanja wetu,” alisema Idd.

Mchezo huo ambao ni wa raundi ya pili kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi, utachezeshwa na waamuzi kutoka Benin ambao ni Adissa Abdul Raphiou Ligali atakayesimama katikati akisaidiwa na Médégnonwa Romains Agbodjogbe na Babadjide Bienvenu Dina.

Na Denis Mtima/GPL

Comments are closed.