The House of Favourite Newspapers

Shilole Ajivisha Pete ya Uchumba

Nuh Mziwanda na Shilole.

Na Mwandishi Wetu/GPL

STAA wa Filamu za Kibongo, Zuwena Mohammed ameamua kujivisha pete ya uchumba mwenyewe, kitendo ambacho kimezua minong’ono kwa watu wengi wakidai kuwa amevishwa na mtu ambaye hajamuweka wazi.

Shilole.

Akizungumza na Ijumaa, Shilole alisema kuwa aliwahi kuvishwa pete na aliyekuwa mpenzi wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’, ikapotea kitatanishi kisha Nuh akaoa mwanamke mwingine hivyo akaona kuliko kidole hicho kibaki tupu, akisitiri.

Nuh Mziwanda.

“Pete ile ya Nuh ilipotea, sijui huwa ni za mashetani? Nimeona ninunue nyingine niivae, hakuna cha mwanaume wala nini, mimi sijaona tatizo kuivaa na huenda ndiyo naiita ndoa,” alisema Shilole.

Comments are closed.