The House of Favourite Newspapers

Nay: Basata Walinirudisha Sana Nyuma

0
Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.

MKALI wa michano ambaye anakimbiza kwenye gemu la Muziki wa  Bongo Fleva kwa sasa na Wimbo wa Wapo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amefunguka kuwa miongoni mwa vitu vilivyomrudisha nyuma kimuziki asiwe mbali zaidi ya hapo alipo ni kufungiwa kwa baadhi ya nyimbo zake pamoja na yeye mwenyewe na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Akichonga na Uwazi Showbiz, wikendi hii Nay alifunguka kuwa Basata walimjeruhi zaidi walipoufungia wimbo wake wa Pale Kati Patamu maana walisababisha akakosa dili la ubalozi alilotakiwa kulipwa shilingi milioni 50, lakini pia takriban shilingi milioni 30 alizotumia kuandaa video ya wimbo huo hazikurudi.

“Kiukweli Basata sometimes wananijeruhi sana wanavyokuwa wanazifungia nyimbo zangu, unajua Basata wanatakiwa kuelewa kuwa mimi ninapokuwa nimeachia wimbo mpya watu wengi wanatamani kuusikia, sasa wanaposikia na kuanza kujadili mambo mengi yanasemwa, wasisikilize hayo, wenyewe wasimame katika misingi ya kazi yao tu basi hapo wataonekana watendaji wazuri zaidi,” alisema Nay.

Leave A Reply