The House of Favourite Newspapers

Tiny Aipigania Ndoa Yake na T.I

0

Na MWANDISHI WETU| GAZETI LA IJUMAA| SHOWBIZ MAMTONI

MKE wa mkali wa Muziki wa Hip Hop, Clifford Harris ‘T.I’, Tiny ameamua kuipigania ndoa yake baada ya kumshambulia kwa maneno kwenye Mtandao wa Instagram msichana anayedaiwa kuchepuka na mumewe, Bernice Burgos.

Kwa mujibu wa mtandao mmoja, Tiny anajaribu kuirudisha ndoa yake kwenye mstari na kwamba hakubaliani na uhusiano mpya wa mumewe na Bernice ulioanzishwa hivi karibuni.

Katika mtandao huo wa Instagram, Tiny alichukizwa na Bernice baada ya kumkejeli kwa kuandika mashairi ya wimbo mmoja wa T.I huku akicheka kwa dharau.

 

Leave A Reply