The House of Favourite Newspapers

Nay Ageukia Ufugaji wa Kuku!

0

Makala: Boniphace Ngumije na Ally Katalambula | GAZETI LA IJUMAA

KUFUATIA mambo mengi kumtokea Mwanamuziki Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ tangu aachie wimbo wake wa Wapo, jamaa ameamua kubadilisha mfumo wa maisha yake ya kila siku.

Utakumbuka hivi karibuni NaY alielezea vitisho vya kuuawa anavyovipata kutoka kwa watu wasiojulikana ambao wanaonesha kutofurahishwa na tamko la Rais Dk. John Magufuli la kutaka aachiwe licha ya wimbo wake kuonekana una ukakasi.

Hata hivyo, kufuatia tukio hilo, dizaini kama jamaa ameamua kutojichanganya sana kitaa, badala yake inadaiwa na watu wake wa karibu kuwa, amekuwa akitulia nyumbani kwake akifanya shughuli za hapa na pale ikiwa ni pamoja na kufuga kuku wake wa kienyeji.

Kusikia hivyo, mapaparazi wetuwakamfungia safari hadi nyumbani kwake, Kimara Mwisho jijini Dar ambapo katika hali ya kushangaza, palikuwa pametawaliwa na ukimya ndipo baadaye ikabainika kuwa, watu aliokuwa anaishi nao akiwemo mama yake, wameondoka kwa hofu ya kufanyiziwa.

HUYU HAPA NAY Baada ya kubisha hodi kwa muda mrefu, alifi ka getini kijana mmoja ambaye kabla ya kufungua aliuliza maswali kibao ndipo alipokwenda kumuita baba mwenye nyumba (Nay).

Alipokuja Nay na kuona ni waandishi anaowafahamu akafungua. Akizungumzia maisha yake kwa sasa, msanii huyo alisema:

“Ni kweli hali yangu ya usalama haipo vizuri, sasa ili kujiepusha na mambo mengine inanilazimu kukaa nyumbani muda mwingi na kufanya shughuli kama hizi za kulisha kuku wangu, kuhudumia garden na shughuli nyingie ndogondogo.

“Kwa kifupi mimi ni mfugaji mzuri sana wa kuku wa kienyeji, ninao wengi na wamenizoea kwa kuwa ni wa kienyeji lakini nawalisha kizungu kama unavyoona.”

Leave A Reply