The House of Favourite Newspapers

Zitto Kabwe Awapinga Mnyika, Lema Kuhusu Miswada ya Dharula ya Madini Kujadiliwa Bunge

0

Jana miswada mitatu inayohusu madini ilisomwa bungeni kwa mara ya kwanza jana. Miswada hiyo iliwasilishwa kwa hati ya dharura kama ambavyo Rais Magufuli aliliomba Bunge  lipitie upya sheria na mikataba ya madini. Bunge pia limeongezwa muda hadi July 5.

 

Wakati anapokea ripoti ya pili ya Kamati Maalumu ya Uchumi na Sheria kuhusu Taarifa ya Makinikia, Rais Magufuli aliliomba Bunge kupitia upya sheria na mikataba yote ya madini na gesi ili kuiepusha nchi kuingia katika mikataba mibovu.

 

Baada ya kuwasilishwa kwa miswada hiyo jana, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika (Chadema)  aliomba mwongozo wa Spika, ambapo aliliomba bunge kuondoa hati ya dharura ya kujadili miswada hiyo.

 

“Muda mfupi uliopita tumekabidhiwa ratiba ya bunge, serikali inaleta miswada mitatu kwa hati ya dharura, mwaka 1997 mikataba ya madini ilipitishwa haraka haraka, mikataba ya ngesi hivyo hivyo,

 

 “Kazi ya bunge ni kutunga sheria, sisi ndio wawakilishi wa wananchi, kwa umuhimu wake na maslahi kwa wananchi, sisi wawakilishi tulitakiwa kukutana na wananchi, hivyo ni bora ikasomwa leo kwa mara ya kwanza na hati ya dharura ikaondolewa na kuletwa bunge lijalo.

 

“Kwa maelezo uliyotoa wadau wataitwa kwa short notice wafike Dodoma kujadili, sisi wabunge vile vile, miswada mitatu inaletwa tuichambue. Huu ni mtego kwa kutufanya tushindwe kuishauri serikali kwa kazi yetu ya kibunge”. Alisema Mnyika

 

Baada ya kauli hiyo ya Mnyika aliyoitoa jana Bungeni, leo Zitto Kabwe(Mbunge wa Kigoma-ACT Wazalendo) amepingana na kauli hiyo  ambapo amesema  Hoja ya hati ya dharura anayoizungumzia Mnyika  ni dhaifu kwa sasa.

==>Huu ni ujumbe wake aliouandika kupitia ukurasa wake Facebook

Lema, Mnyika Waliamsha Tena Dude Bungeni

Leave A Reply