The House of Favourite Newspapers

Kumbe Hata Ajibu na Chirwa

Ibrahim Ajibu (Katikati) akifanya yake kimataifa.

KWA mujibu wa takwimu za umri wa wachezaji wa Yanga, zilizoko kwenye ofisi za CAF pale Misri ni kwamba kabla hata Ibrahim Ajibu na Obrey Chirwa hawajazaliwa, Yanga haikuwahi kupata rekodi nzuri mwezi huu wa Aprili dhidi ya Simba.

 

Uongozi wa Yanga umeiambia CAF kwamba wachezaji hao ni miongoni mwa wachezaji wake waliozaliwa baada ya 1992, jambo ambalo kwa hesabu za kawaida linamaanisha kwamba hawajafikisha miaka 26 ya kuzaliwa.

Obrey Chirwa

Tangu 1992, Simba na Yanga kwenye Ligi Kuu Bara zimekutana mara saba mwezi Aprili, Yanga imeshinda mara moja tu huku Simba ikiibuka kidedea mara mbili. Zilizobaki ni droo na suluhu.

Chirwa na Ajibu ndiyo nyota wa Yanga kwenye mechi ya leo dhidi ya Simba, ambao rekodi za CAF zinadai Ajibu ana miaka 21 huku mwenzie akiwa na 24. Wachezaji wa Yanga ambao wamezaliwa kipindi hicho, takwimu zinasema kwamba walikuwa hawajazaliwa ni Pato Ngonyani,Hassan Kessy,Abdallah Shaibu, Andrew Vincent na Gadiel Michael.

STORI NA IBRAHIM MRESSY

Comments are closed.